Responsive image
Responsive image
Posted : February 22, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Eneo la Tanganyika nchini Congo ambalo wakazi wake wanakabiliwa na janga la kibinadamu
Responsive image

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limeonya kuwa wakazi wa eneo la Tanganyika, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, wako katika hatari ya kukabiliwa na janga la kibinadamu.

UNHCR imesema wakazi wa eneo hilo wamejikuta wakiwa katika njiapanda baada ya eneo lao kukabiliwa na mapigano makali na wengi wao kulazimika kukimbilia katika nchi jirani.

Shirika hilo limesema usalama mdogo katika jimbo hilo la Tanganyika, linasababisha misaada ya kibinadamu kushindwa kuwafikia watu wanaohitaji haraka.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment