Responsive image
Responsive image
Posted : February 22, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Moja ya maeneo ya mapigano nchini Syria
Responsive image

Idadi ya watu waliokufa kutokana na mashambulio yanayofanywa na majeshi ya serikali dhidi ya waasi katika eneo la kusini mwa Ghouta, nchini Syria imefikia 250. 

Majeshi ya serikali ya Syria yakishirikiana na  majeshi ya nchi washirika yameendelea kufanya mashambulio zaidi katika eneo hilo, huku waathirika wakubwa wakiwa ni raia.

Licha ya mashambulio makali katika eneo hilo yanayofanywa na majeshi ya serikali ya nchi hiyo kwa msaada wa majeshi ya Russia, wakazi wa eneo hilo, pamoja na waasi wamesema hawako tayari kuyakimbia makazi yao.

Haya ni mashambulio mabaya zaidi kuliko yote kuwahi kutokea na kuumiza raia nchini Syria, tangu mwaka 2013.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment