Responsive image
Responsive image
Posted : February 17, 2018 (a month ago) By TBC
Responsive image
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage
Responsive image

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Jaji Semistocles Kaijage amesema mawakala ambao wamefika vituoni wakiwa na hati mbili tofauti za kusimamia uchaguzi wamekosa sifa ya kisheria ya kusimamia vituo. 

Jaji Kaijage ameyasema hayo kutokana na baadhi ya mawakala wa vyama vya siasa katika majimbo ya Siha na Kinondoni kufika vituoni na kubainika fomu za viapo vyao kuwa na kasoro hivyo kunyimwa kuendelea na zoezi la usimamizi.

Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni Aron Kagurumjuli amesema kuna mawakala ambao wamekosa fomu kutokana na viongozi wa vyama kutofuata fomu hizo mapema pamoja na barua za utambulisho vituoni. 

Uchaguzi wa marudio Jimbo la Kinondoni na Siha unafanyika kufuatia wabunge wa majimbo hayo kujiuzulu. 

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment