Responsive image
Responsive image
Posted : February 16, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Donald Trump wa Marekani
Responsive image

Siku moja baada ya wanafunzi 17 kuuawa kwa kupigwa risasi huko Miami, Florida nchini Marekani, Chama cha Democrat kimewashutumu Rais Donald Trump na Spika wa bunge la nchi hiyo Paul Ryan kwa kukataa kuruhusu mjadala wa sheria ya kumiliki silaha.

Wamarekani bado wanaendelea kuomboleza vifo vya wanafunzi 17 waliouawa kwa kupigwa risasi na mtu anayeshukiwa kuwa kijana aliyewahi kusoma shuleni hapo na kufukuzwa kwa utovu wa nidhamu. Tangu kutokea kwa tukio hilo, ambalo si la kwanza nchini Marekani,  pamekuwa na wito kwa nchi hiyo kubadili sheria ya kumiliki silaha.

Akizungumzia mauaji hayo Rais wa Marekani Donald Trump awali katika hotuba yake amesema usalama katika shule utakuwa ni moja ya mambo yatakayopewa kipau mbele lakini alishindwa kulishauri bunge la nchi hiyo lipitie upya sheria ya kumiliki silaha.

Wakati huo huo shughuli ya kuwasha mishumaa kuwakumbuka waliouawa kwenye tukio hilo imefanyika huko Florida kulikotokea tukio hilo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment