Responsive image
Responsive image
Posted : February 14, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli
Responsive image

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. John Magufuli amemteua Meja Jenerali Yakubu Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema pamoja na uteuzi huo, Rais Magufuli amempandisha cheo mnadhimu huyo mpya kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali. Luteni Jenerali Mohamed amechukua nafasi ya Luteni Jenerali James Mwakibolwa ambaye amestaafu.

Rais Magufuli pia amewapandisha vyeo mabrigedia Jenerali 10 kuwa Meja Jenerali.

Waliopandishwa vyeo ni pamoja na Brig Jen Kingu, Brig Jen Busungu, Brig Jen. Mrangira, Brig Jen Masanja, Brig Jen. Msongole, Brig Jen Kapinga, Brig Jen Njelekela, Brig Jen. Bahati, Brig Jen Mkingule na Brig Jen Makona. Mabrigedia Jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye.

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Mohamed ataapishwa kesho Ikulu Dar es salaam.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment