Responsive image
Responsive image
Posted : February 14, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Responsive image

Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa amesema serikali imeongeza vituo vya afya hapa nchini kutoka  6521 mwaka 2010 hadi  vituo vya  afya  7680 mwaka 2016, idadi ambayo ni ongezeko kubwa katika jitihada za serikali kuboresha huduma ya afya nchini.

Akizungumza katika uzinduzi wa jengo jipya la utoaji huduma ya mama na mtoto katika Hospitali ya Amana jijini DSM, Waziri  Mkuu amesema serikali imeendelea kuboresha vituo vya afya.

Awali akizungumza  katika  uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa DSM , Paul Makonda amesema serikali ya Mkoa wa DSM itahakikisha  hospitali za mkoa huo zinatoa huduma bora zaidi ili kuwasaidia wananchi kuondokana na usumbufu wa kulazimika kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment