Responsive image
Responsive image
Posted : February 14, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro
Responsive image

Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni limethibitisha kuokotwa kwa mwili wa mtu mmoja mwenye jinsia ya kiume ukiwa na majeraha katika ufukwe wa Coco jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Jumanne Muliro amesema uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo.

Katika hatua nyingine Kamanda Muliro amesema Polisi mkoani kwake wamejipanga kuhakikisha uchaguzi wa marudio katika jimbo la Kinondoni unafanyika kwa amani. Uchaguzi wa marudio katika Jimbo la Kinondoni unatarajiwa kufanyika Jumamosi Februari 17.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment