Responsive image
Responsive image
Posted : February 14, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Mwanafunzi aliyekatishwa masomo na baba yake na kuozeshwa
Responsive image

Baba mlezi wa mwanafunzi mmoja wa darasa la pili wilayani Same mkoani Kilimanjaro amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlazimisha mtoto huyo kukatisha masomo na kuolewa.

Akizungumzia tukio hilo Afisa ustawi wa jamii wilayani Same, Lucy Venance amesema baadhi ya wazazi wamekuwa mstari wa mbele kukwamisha jitihada za watoto wao kuendelea na masomo.

Katika kipindi cha mwaka 2017, Halmashauri ya wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro imepokea matukio manne ya watoto wa kike kutaka kuozeshwa ambapo watuhumiwa watatu walitoroshwa licha ya watoto waliofanyiwa ukatili huo kuokolewa.

Kituo cha Ushauri Same ambacho kinamhudumia mwanafunzi huyo kwa sasa kimeitaka jamii kushirikiana kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu na kutimiza ndoto zao.

TBC ilizungumza na Mwendesha mashtaka katika mahakama ya wilaya ya Same, Ancibetus Kechoka ambaye amekiri kupokea shtaka hilo ambapo mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka thelathini huku katibu tawala wa wilaya ya Same, Sospeter Magonera akielezea azma ya kuendelea kuwatafuta wazazi wa mtoto huyo.

SAUDA SHIMBO

13 FEBRUARI 2018

 

 

 

 

 

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment