Responsive image
Responsive image
Posted : February 14, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Wadau wa habari wakisikiliza mada kuadhimisha Siku ya Radio duniani
Responsive image

Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya radio ambapo wadau wa sekta ya mawasiliano kwa umma wametoa wito kwa wamiliki wa vyombo hivyo kuajiri watu wenye taaluma ya uandishi wa habari wanaofanya kazi kwa weledi kuelimisha jamii.

Baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam wamesema pamoja na kukua kwa teknolojia ikiwemo uwepo wa mitandao ya kijamii radio imeendelea kuwa chombo cha habari chenye nguvu katika kuhabarisha.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) mpaka sasa radio zilizosajiliwa hapa nchini ni 152, TBC Taifa ikiwa ndiyo radio kongwe ambapo uwepo wake ni wa takribani miaka 62.

Siku ya radio duniani huadhimisha kila Februari 13 kwa lengo la kuendelea kueleza umuhimu wa radio kwa jamii.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment