Responsive image
Responsive image
Posted : February 14, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Zoezi la bomoa bomoa linaloendeshwa na Manispaa ya Dodoma
Responsive image

Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imeanza zoezi la kubomoa nyumba zinazojengwa katikati ya mji bila kufuata taratibu za ujenzi zinazotolewa na Manispaa hiyo.

Zoezi hilo limekuja kufuatia baadhi ya wananchi waliopewa vibali vya ukarabati na Manispaa hiyo kugeuza matumizi ya vibali hivyo na kuvitumia katika ujenzi.

Akiongoza utekelezaji wa zoezi hilo, Mkuu wa oparesheni Ally Bera amesema zoezi hili ni endelevu ili kuhakikisha hakuna ujenzi holela utaofanyika katika manispaa hiyo. 

Bera ametoa rai kwa yeyote anayetaka kujenga katika Manispaa ya Dodoma kuhakikisha ana kibali cha ujenzi.

Baadhi ya wananchi walioshuhudia ubomoaji wameunga mkono zoezi hilo na kutaka liwe la endelevu.

 ANETH ANDREW

13 FEBRUARI 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment