Responsive image
Responsive image
Posted : February 13, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mathias Kagulugulu
Responsive image

Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imesema hakuna mtumishi yoyote kati ya walioondolewa kutokana na kubainika kuwa na vyeti vya kughushi anayeidai serikali.

Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mathias Kagulugulu katika kikao cha viongozi waliochini ya ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI.

Awali akifungua kikao hicho Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo amewataka watendaji hao kutojifanya miungu watu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe ametaka Maafisa Utumishi Nchini kuwa na uchungu katika kutatua kero za wafanyakazi.

ANETH ANDREW

FEBRUARI 13, 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment