Responsive image
Responsive image
Posted : February 13, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina
Responsive image

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ameagiza kuchukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi watumishi waliothibitika kujihusisha na uvuvi haramu wakati wa utekelezaji wa operesheni ya kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu nchini.

Katika operesheni hiyo iliyodumu kwa siku 40 serikali imekusanya shilingi Bilioni 4.7 kutokana na faini walizotozwa wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara wa mazao ya samaki waliopatikana na makosa yanayohusu uvuvi haramu.

Waziri Mpina amesema atahakikisha baada ya muda mfupi uvuvi haramu unakuwa historia kufuatia operesheni ya kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu awamu ya kwanza kupata mafanikio.

Akizungumza katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa operesheni hiyo kilichofanyika jijini Mwanza Waziri Mpina amesema wamebaini kuwa uvuvi haramu umeshamiri kutokana na viongozi waliopewa dhamana kujihusisha na uvuvi haramu.

Operesheni hiyo ya kitaifa dhidi ya uvuvi haramu awamu ya kwanza imehusisha wizara za Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

REGNALID NDESIKA

FEBRUARI 13, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment