Responsive image
Responsive image
Posted : February 12, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
Responsive image

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema serikali itaendelea kulinda na kuhifadhi kumbukumbu za kihistoria hapa nchini kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipotembelea na kukagua uboreshaji wa jengo lililokuwa Makao Makuu ya Kamati ya ukombozi wa nchi za Afrika na baadaye kukabidhiwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama makumbusho ya historia.

Dkt. Mwakyembe amewaomba wananchi kulinda na kutunza maeneo yenye ishara za kumbukumbu ya harakati za ukombozi wa bara la Afrika na kutoa taarifa kwa wizara husika ili kutunza maeneo hayo.

Tanzania imeteuliwa kuwa Makao makuu ya kumbukumbu za harakati za ukombozi wa bara la Afrika na kituo hicho kinajengwa Jijini Dar es salaam .

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment