Responsive image
Responsive image
Posted : September 18, 2017 (8 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa mambo ya nje nchini Marekani , Rex Tillerson
Responsive image

Waziri wa mambo ya nje nchini Marekani , Rex  Tillerson amesema serikali ya Marekani inaweza kuanza kujihusisha upya na makubaliano ya kimataifa ya kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi, licha ya Rais wa nchi hiyo Donald Trump kutangaza kwamba ataitoa nchi hiyo nje ya mkataba wa Paris

Tillerson  amesema Marekani inaouwezo wa kuanza  kujadili mkataba huo kwa masharti yatakayoweza kufaa zaidi taifa lake .

Hatahivyo  mshauri wa masuala ya usalama wa Taifa nchini Marekani , H.R McMaster amesema Rais Trump  kwa sasa yuko wazi kwa mazungumzo yoyote ambayo yataweza kuimarisha masuala ya mazingira.

Katika hatua nyingine, Tillerson amesema serikali yake inaendelea kujadili mpango wake wa  kufunga ubalozi wake nchini Cuba , baada ya kutokea  kwa mlolongo wa mashambulizi ya kelele kwa wafanyakazi wake.

Mpaka sasa zaidi ya wafanyakazi 20 walioko  ubalozi wa Marekani nchini Cuba  wameripotiwa kuwa na matatizo ya afya ya ubongo na wengine wakipoteza uwezo wa kusikia kutokana na mashambulizi hayo.

Hatahivyo serikali ya Marekani  imeiambia Havana kwamba jukumu la kuwalinda wafanyakazi wake walioko nchi nyingine lipo juu yao.

Uchunguzi zaidi unaendelea kujua chanzo cha watu hao kutosikia.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment