Responsive image
Responsive image
Posted : September 14, 2017 (8 months ago) By TBC
Responsive image
Baadhi ya madhara ambayo yamesababishwa na kimbunga cha Irma nchini Marekani.
Responsive image

Habari kutoka nchini Marekani zinasema, hadi sasa kimbunga Irma kilichoipiga nchi ya Marekani na visiwa vya Caribbean kimesababisha vifo vya watu 77 nusu yao wakiwa ni kutoka nchini Marekani.

 

Miongoni mwa watu waliokuwa kutokana na kimbunga Irma ni watu wanne kutoka katika kituo cha kulele wazee cha Holy Wood kilichoko katika jimbo la Florida, jimbo ambalo lilipigwa vibaya na kimbunga hicho.

 

Wachunguzi wa masuala ya usalama wakati wa kimbunga wanasema, bila shaka watu hao walikufa baada ya kukosa hewa au kupata joto kali baada ya kituo hicho kukosa huduma ya umeme. Huduma ya umeme ililazimika kukatwa katika maeneo mengi ya jimbo la Florida ili kupisha athari za kimbunga Irma.

 

Habari zinasema wagonjwa watatu walikuwa wakiwa wamekufa ndani ya kituo hicho cha kulelea wazee na wengine watano walikufa baada ya kufikishwa hospitalini.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment