Responsive image
Responsive image
Posted : September 14, 2017 (8 months ago) By TBC
Responsive image
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un.
Responsive image

Korea Kaskazini imesema itachukua hatua kali zaidi katika majaribio yake ya nyuklia baada ya kuwekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa.

 

Nchi hiyo imesema vikwazo hivyo vinaikwamisha nchi hiyo kupiga hatua mbalimbali za kimaendeleo, hivyo imepanga kuchukua hatua kali zaidi hasa dhidi ya Marekani.

 

Korea Kaskazini imesema hatua itakazochukua dhidi ya Marekani zitakuwa ni kubwa kulikozozote zilizowahi kuchukuliwa na taifa lolote dhidi ya nchi hiyo, tangu taifa hilo lilipoanzishwa na ni tukio ambalo Marekani haitalisahau.

 

Naye Rais Donald Trump wa Marekani amesema, vikwazo ilivyowekewa Korea Kaskazini ni vidogo na hiyo ni moja kati ya hatua ndogo sana za kuishikisha nchi hiyo adabu, baada ya kuendelea na mpango wake wa nyuklia.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment