Responsive image
Responsive image
Posted : September 13, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
Responsive image

Rais John Magufuli ameuvunja Wakala wa Uendelezaji Mji wa Kigamboni -KDA kuanzia leo na kuelekeza shughuli zote za wakala huo zifanywe na manispaa ya Kigamboni jijini Dar Es Salaam.

Akitangaza uamuzi huo kwa niaba ya Rais, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi pia amefuta mashamba mawili baada ya wamiliki wake kushindwa kuyaendeleza na kuwanyima fursa wananchi kufanya shughuli zingine.

Kwa upande wake mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile na baadhi ya wananchi  wamepongeza hatua hiyo kwa maelezo kwamba wamekuwa wakipata ugumu wa kuendeleza maeneo yao kutokana na urasimu wa KDA.

 

13 Septemba 2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment