Responsive image
Responsive image
Posted : September 13, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Barnabas Mwakalukwa
Responsive image

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Barnabas Mwakalukwa amewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii kuacha kuchangia taarifa zenye muelekeo wa uchochezi zinazotolewa na baadhi ya watumiaji wa mitandao hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mwakalukwa amesema taarifa zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii pamoja na picha za askari wa jeshi hilo kuonekana Nairobi nchini Kenya kuwa anafutilia taarifa za Tundu Lissu hazina ukweli wowote.

Amesema jeshi la polisi kupitia kitengo cha upelelezi wa makosa ya kimtandao linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wote waliohusika na kusambaa kwa taarifa hizo za uongo ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Pia jeshi hilo limewatahadharisha wananchi waache kutumia mitandao ya kijamii vibaya na badala yake mitandao hiyo itumike kuelimisha na kuihabarisha jamii juu ya masuala mbalimbali ya maendeleo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment