Responsive image
Responsive image
Posted : September 13, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Spika wa Bunge Job Ndugai
Responsive image

Spika wa Bunge Job Ndugai ameiagiza Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, pamoja na Kamati ya MaadiliHaki na Madaraka ya Bunge kumhoji mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea kwa madai kuwa Spika amelidanganya bunge kuhusu tukio la kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Spika Ndugai ametoa agizo hilo bungeni mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu ambapo pia ameitaka kamati ya Maadili kumhoji Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto kwa lugha alizotumia kuhoji mhimili wa bunge mtandaoni.

Katika hatua nyingine, bunge limepitisha muswada wa sheria wa marekebisho ya sheria mbalimbali namba 3 wa mwaka 2017.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment