Responsive image
Responsive image
Posted : September 12, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli akimjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania -JWTZ, Lugalo.
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli ametembelea hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania -JWTZ Lugalo, Jijini Dar es salaam  na kumjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni Jijini Dar es salaam.

 

Meja Jenerali Mstaafu Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana majira ya mchana na kisha kukimbizwa katika hospitali ya Jeshi Lugalo kwa matibabu.

 

Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe amemueleza Rais Magufuli kuwa Meja Jenerali Mstaafu  Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa risasi alizopigwa mkononi, kiunoni na tumboni.

 

Meja Jenerali Mstaafu MRITABA amemshukuru Rais Magufuli kwa kumjulia hali na kumuombea dua ili apone haraka.

 

Rais Magufuli aliyeongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jen. Venance Mabeyo pia ametembea wodi ya majeruhi na kuwajulia hali wagonjwa wanaotibiwa katika wodi hiyo na baadaye akawasalimu wananchi waliofika hospitali hapo kwa ajili ya kupata matibabu.

 

Dkt. Magufuli amewapongeza Madaktari wa hospitali ya jeshi Lugalo kwa huduma za matibabu wanazotoa kwa askari na wananchi wengine na amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment