Responsive image
Responsive image
Posted : September 12, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli
Responsive image

Rais Dkt.John Magufuli amesaini na kupitisha muswada minne  ya sheria ukiwemo muswada ya  marekebisho ya sheria mbalimbali namba tatu kuwa sheria kamili.

 

Hayo yamesemwa Bungeni Mjini Dodoma na Spika wa Bunge Job Ndugai mud mfupi kabla ya kuanza kwa kipindi cha Maswali na Majibu.

 

Baada ya taarifa hiyo kipindi cha maswali na majibu kikaendelea ambapo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia wazee na watoto, Dkt.Khamisi Kigwangala amesema serikali itanunua mashine tatu za kupima vinasaba -DNA ili kupunguza usheleweshaji wa majibu.

 

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Yusuph Masauni amesema serikali inafanya kila jitihada kupunguza idadi ya wakimbizi hapa nchini.

 

Wakati huo huo waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema serikali itajenga nyumba za wanajeshi elfu kumi nchi nzima ambapo kwa awamu ya kwanza imejenga nyumba elfu sita kwa Tanzania Bara na Ghorofa 40 upande wa Zanzibar.

 

 

DARLIN SAID

SEPTEMBA 12, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment