Responsive image
Responsive image
Posted : September 05, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Kiongozi wa Muungano wa NASA nchini Kenya Raila Odinga
Responsive image

Kiongozi wa Muungano wa NASA nchini Kenya Raila Odinga  amesema hatakuwa tayari kushiriki uchaguzi mkuu wa marudio uliopangwa na  tume ya  uchaguzi nchini humo Octoba 17 2017.

Odinga amesema kuwa anataka kuwepo mikakati ya kisheria na kikatiba, kabla ya yeye kukubali kushiriki uchaguzi huo.

Aidha Odinga ametaka mabadiliko ya kisheria kufanyika katika Tume ya Uchaguzi nchini humo, ambayo imelaumiwa na mahakama ya juu kwa wa kuendesha uchaguzi kwa njia ambayo haiukuwa nzuri ambayo ilisababisha kufutwa kwa matokeo.

Jana Jumatatu Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya ilitangaza kwamba uchaguzi mpya wa urais nchini humo utafanyika tarehe 17 Oktoba.

Kwa mujibu wa Tume  ya Uchaguzi ya taifa hilo wagombea wawili pekee wa urais, Rais Uhuru Kenyatta na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga ndiyo watachuana kwenye kinyang’anyiro hicho.

 

SEPTEMBA 05, 2017

CHANZO BBC

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment