Responsive image
Responsive image
Posted : September 04, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga kutoka muungano wa NASA.
Responsive image

Uchaguzi wa marudio nchini Kenya umepangwa kufanyika Oktoba 17 mwaka huu.

Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini humo – IEBC imesema uchaguzi huo utahusisha wagombea wawili wa kiti cha urais ambao ni Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga kutoka muungano wa NASA.

Mahakama ya Juu nchini Kenya Septemba Mosi mwaka huu ilibatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais nchini humo na kuiagiza IEBC kufanya uchaguzi wa marudio ndani ya siku 60 tangu kubatilishwa kwa matokeo hayo.

04 Septemba 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment