Responsive image
Responsive image
Posted : September 04, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga
Responsive image

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema  Muungano wa upinzani NASA hautokubali kugawana madaraka, kauli ambayo ameitoa ikiwa ni siku kadhaa baada ya Mahakama Kuu kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Rais uliofanyika mwezi uliopita na kutoa amri ya kuitishwa uchaguzi mwengine ndani ya siku 60.

 

 Mahakama Kuu imesema Ijumaa kwamba tume ya uchaguzi ilifanya makosa yaliyobatilisha uchaguzi wa Agosti 8 na kufuta ushindi wa kura milioni 1.4 wa Rais Uhuru Kenyatta aliyekuwa madarakani.

 

Kufuatia amri hiyo ya mahakama mvutano umeanza kupamba moto kati ya kambi mbili za Kenyatta mwenye umri wa miaka 55, na Odinga mwenye miaka 72.

 

Kenyatta amesisitiza kwamba uchaguzi ufanyike tena chini ya usimamizi wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (IEBC) ambapo upinzani umepinga hilo.

 

Odinga ameitaka tume ya IEBC ijiuzulu na pia ifunguliwe mashtaka ya makosa ya jinai.

 

 

Chanzo DW.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment