Responsive image
Responsive image
Posted : September 02, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Rais wa Uhuru Kenyatta wa Kenya
Responsive image

 Rais wa Uhuru Kenyatta wa Kenya  amewaita majaji wa Mahakama ya juu ya nchi hiyo wadanganyifu baada ya kubatilisha matokeo yake ya ushindi wa uchaguzi wa urais.

Mapema jana Kenyatta aliwataka watu kuwa watulivu na kusema anaheshimu maamuzi ya mahakama hiyo.

 Mahakama ya juu imegundua kasoro katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita na kuagiza kurudiwa ndani ya siku 60.

Kamati ya Uchaguzi nchini Kenya ilimtangaza Kenyatta mshindi kwa tofauti ya kura milioni 1.4 lakini matokeo hayo yalipingwa mahakamani na mpinzani wake Raila Odinga.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment