Responsive image
Responsive image
Posted : September 01, 2017 (8 months ago) By TBC
Responsive image
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Responsive image

Kenyatta: Nipo tayari kwa uchaguzi wa marudio

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema baada ya mahakama ya juu nchini humo kutangaza kwamba  uchaguzi wa  Urais urudiwe ndani ya siku 60 yeye pamoja na chama chake wapo tayari kwa uchaguzi huo.

Kenyatta  ametoa kauli hiyo muda mchache baada ya Mahakama ya juu kutoa maamuzi ya kesi iliyofunguliwa na Muungano wa NASA ukiongozwa  na Raila Odinga kupinga ushindi wa Rais Kenyatta uliotangazwa baada ya uchaguzi wa  taifa hilo Agosti 08 2017.

“Tupo tayari kwa debe , turudi tuwaeleze wakenya wao wataamua ila  jambo kubwa la msingi ni Amani, Amani, Amani” Amesema Rais Kenyatta.

Katika hukumu liyosomwa mapema leo na Jaji Mkuu wa Mahakama ya juu  Kenya, Jaji David Maraga amesema mahakama hiyo inayoundwa na majaji saba imeridhika kuwa tume ya uchaguzi ya kenya ilikiuka sheria ya uchaguzi wa nchi hiyo kwa kutokutimiza masharti ya kutayarisha na kuendesha uchaguzi.

 

 

GODFRIEND MBUYA

SEPTEMBA MOSI

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment