Responsive image
Responsive image
Posted : September 01, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Jaji Mkuu wa Mahakama ya juu Kenya David Maraga
Responsive image

  

Mahakamu ya juu chini  Kenya imefuta matokeo ya Urais ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo tarehe nane, mwezi wa nane mwaka huu.

Katika hukumu liyosoma mapema leo na Jaji Mkuu wa Mahakama ya juu  Kenya, Jaji David Maraga amesema mahakama hiyo inayoundwa na majaji saba imeridhika kuwa tume ya uchaguzi ya kenya ilikiuka sheria ya uchaguzi wa nchi hiyo kwa kutokutimiza masharti ya kutayarisha na kuendeshauchaguzi 

Katika uchaguzi huo Rais aliyemaliza muda wake, Uhuru Kenyatta aliwashinda wagombea wengine Saba akiwemo kinara wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga aliyegombea kwa tiketi ya muungano wa upinzani wa NASA.

Uchaguzi mpya kwa nafasi ya urais unatarajia kufanyika tena ndani ya siku 60 tangu hukumu kamili itakapotolewa.

 

Grolia Michael

Septemba 01,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment