Responsive image
Responsive image
Posted : August 23, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Mwanasoka bora duniani Cristiano Ronaldo
Responsive image

Mwanasoka bora duniani kwa sasa Cristiano Ronaldo amesema kitendo cha mamlaka za soka nchini Hispania kutupilia mbali rufaa iliyokatwa na klabu yake ya Real Madrid ya yeye kufungiwa michezo mitano ni dhuluma dhidi yake.

Hapo jana kamati ya nidhamu ya michezo nchini Hispania ilitangaza kutupilia mbali rufaa ya nyota huyo mwenye maiaka 32 baada ya kutolewa nje kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano kwenye ushindi wa timu yake wa magoli matatu kwa moja dhidi ya mahasimu wao barcelona kwenye mchezo wa kwanza wa Spain Super Cup.

kupitia ukurasa wake wa instagram, ronaldo ameandika “ maamuzi mengine yasiyoeleweka, dhuluma juu ya dhuluma hawataweza kamwe kunipindua mimi”.

 

Asheri Thomas

Agosti 23,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment