Responsive image
Responsive image
Posted : August 21, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Kiongozi wa kanisa katoliki Ufilipino Kadinali Luis Tagle
Responsive image

Kiongozi wa kanisa katoliki huko Ufilipino Kadinali Luis Tagle ametoa wito kwa serikali nchini humo kumaliza vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya kufuatia vifo vya watu mbalimbali tangu Rais Rodrigo Duterte alipotangaza vita dhidi ya biashara hiyo.

Kiongozi huyo ametoa wito huo katika ibada ya jumapili ya leo nchini humo ambapo amesema watu sabini na sita akiwemo kijana wa miaka kumi na saba wameuawa katika mapambano na jeshi la polisi baada ya Rais Duterte kutangaza kufanyika kwa oparesheni nyingine iliyolenga kukabilina na biashara ya dawa za kulevya katika maeneo mbalimbali ya mji wa Manila huko Ufilipino.

Amesema mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini humo yanapaswa kushirikisha taasisi mbalimbali ikiwemo zile za dini ili kuwafikiwa wananchi wengi na kwa njia salama isiyohatarisha maisha ya watu wengi kwa kutumia silaha za moto.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment