Responsive image
Responsive image
Posted : August 19, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Mashabiki wa timu ya simba
Responsive image

Wakati homa ya mpambano wa ngao ya hisani kati ya Timu ya Soka ya Simba na Yanga siku ya Jumatano Agosti 23 2017 uwanja  wa taifa Dar es salaam ikizidi kupanda kwa mashabiki, Jeshi la polisi limewataka mashabiki hao wa vilabu hivyo kuwa na nidhamu kabla ya mchezo na baada ya mchezo.

Akizungumza na TBC Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lucas Mkondya amesema jeshi hilo lipo imara na watakaokaidi kutii sheria bila shuruti watatiwa mbaroni. 

Mchezo wa ngao ya hisani utaopigwa Agosti 23 unaashiria ufunguzi wa Ligi kuu Tanzania  bara itakayoanza Agosti 26 mwaka huu.

 

GODFRIEND MBUYA

AGOSTI 19, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment