Responsive image
Responsive image
Posted : August 12, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Rais mpya wa TFF Wallace Karia
Responsive image

Mgombea wa kiti cha Urais wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania Wallace Karia  amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Soka hapa nchini - TFF baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa shirikisho hilo uliofanyika mjinini DODOMA baada ya kuwabwaga wapinzani wake watano katika uchaguzi huo.

Karia amepeta kura 95 kati ya kura 130 zilizopigwa huku Ally Mayay Tembele  akipata kura 9 sawa na  Shija Richard aliyepata kura kama hizo yaani kura tisa.

Katibu Mkuu wa zamani wa shirikisho hilo – Fredrick Mwakalebela ameambulia kura 3 , naye mwenyekiti wa zamani wa timu ya Yanga,  Iman Madega amepata kura 8 huku Emmanuel Kimbe akiwa amepata kura 1.

Katika nafasi ya Umakamu wa Rais Michael Wambura amewabwaga wapinzani wake wanne kwa kupata ushindi mnono wa kura 85 na kuwa makamu wa Rais wa Shirikisho hilo ambapo Mulamu Ngh’ambi  amepata kura 25 Richard Selasela  ameambulia kura  mbili na mchezaji wa zamani wa timu ya Simba na timu ya Taifa  Mtemi Ramadhan akiambulia kura 14.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment