Responsive image
Responsive image
Posted : August 12, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Magufuli ampongeza Kenyatta kwa kuchaguliwa kuongoza taifa la Kenya kwa kipindi kingine
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli amemtumia salamu za pongezi Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa kuchaguliwa kuongoza taifa hilo kwa kipindi kingine.

Rais Magufuli ametuma pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo pia amemtakia Kenyatta mafanikio mema.

Kenyatta ametangazwa rasmi kushinda kiti cha urais nchini Kenya Ijumaa Agosti 11 usiku kwa kupata asilimia 54.2 ya kura zote.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amemteua Bernard Konga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya -NHIF.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Konga umeanza tarehe 09 mwezi huu.

Kabla ya uteuzi huo Konga alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

 

12 August 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment