Responsive image
Responsive image
Posted : August 11, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro
Responsive image

Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka wananchi wa  Kibiti mkoani Pwani kuendelea na shughuli za uzalishaji mali na kushiriki katika ibada misikitini na makanisani  kutokana na kuimarika kwa hali ya ulinzi na usalama mkoani humo.

Sirro amesema hayo alipotembelea eneo la KibitiI siku moja baada ya watuhumiwa 13 kufa katika majibizano na polisi  katika eneo la Gari Bovu, kijiji cha Chamiwaleni, Kata ya Mchukwi, Wilaya ya Kibiti, Mkoa wa Kipolisi Rufiji na kusema kuwa hali iko vizuri hivyo wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida. 

IGP Sirro  pia amewapongeza askari wanaoendelea kuimarisha amani na usalama katika eneo hilo na kuahidi jeshi la polisi kuendelea kusimamia sheria. 

 

‚ÄčAngella Msangi                

11/8/2017‚Äč

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment