Responsive image
Responsive image
Posted : August 11, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge
Responsive image

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge ameitaka jamii kuelekeza nguvu katika kuyalinda mazingira kwa lengo la kupambana na janga la tabia nchi.

Akizungumza na Tbc jijini DSM, Waziri Lwenge amesema mapambano ya tabia nchi yanaenda pamoja na ulinzi wa mazingira hususani katika vyanzo vya maji ili jamii iendelee kunufaika na upatikanaji wa maji safi na salama.

Aidha ameitaka Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka mkoa wa Pwani  na Dsm,  kuhakikisha inailinda miundombinu ya maji hususani mitambo ya Maji Ruvu juu na Ruvu chini ili wakazi wa mikoa ya DSM na PWANI waendelee kupata maji safi salama na yenye kutosheleza.

 Amewataka wananchi wafuate utaratibu wa kuomba kuunganishiwa maji na kulipa Ankara zao kwa wakati kwakuwa maji yapo yakutosha.

 

Aron Mrikalia                               

11/8/2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment