Responsive image
Responsive image
Posted : August 11, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba
Responsive image

Waziri Mkuu Mstaafu Jaji  Joseph Warioba amekiagiza Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo –SUA Tawi la Arusha - Olmotonyi kushirikiana na Wakazi wanaozunguka chuo hicho kutunza misitu na kutunza vyanzo vya maji.

Jaji Warioba ambaye ni mkuu wa chuo kikuu hicho ametoa agizo hilo katika chuo cha kilimo na misitu cha Olmotonyi na kuongeza kuwa kwa kuboresha ushirikiano huo utunzaji wa misitu utakuwa endelevu.

Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Warioba anaomba kuwepo kwa ushirikiano baina ya chuo na Wakazi wanaozunguka eneo hilo ili kulinda misitu iliyopo.

Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokokine –Sua tawi la Arusha - Olmotonyi  kina hekari zaidi ya mia nane za misitu na hekari zaidi ya mia sita za miti zilizooteshwa kwa lengo la kutoa elimu kwa wanachuo pamoja na kutunza vyanzo vya maji na mazingira.

 

Sechelela Kongola                   

11/8/2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment