Responsive image
Responsive image
Posted : August 10, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Mwanariadha Emmanuel Ginik
Responsive image

Mwanariadha Emmanuel Giniki ameshindwa kufuzu kwa hatua ya fainali ya michuano ya dunia ya riadha baada ya usiku wa kuamkia leo kumaliza wa mwisho kwenye mbio za mita elfu tano na kumuacha bingwa mtetezi wa mbio hioz – Mo Farah akisonga mbele licha ya kumaliza wa pili.

Pamoja na kuongoza mara kadhaa, Giniki hakuweza kuwa na mwendelezo mzuri kwenye mbio hizo zinazofanyika jijini London, Uingereza na hivyo kushindwa kuendana na kasi ya wakimbiaji wengine.

Baada ya Alphonce Simbu kufanya vizuri kwenye mbio ndefu na kutwaa medali ya Shaba, macho na masikio ya Watanzania yalielekezwa kwa Giniki ili kushuhudia endapo nayeye angeipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Katika hatua hiyo ya nusu fainali ya mbio za mita elfu 5, kundi la Giniki lilikuwa na jumla ya wanariadha 22.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies FashionFabian  |  6 months ago   |   August 24, 2017
"Hilo Jipu Nalo"

Leave Your Comment