Responsive image
Responsive image
Posted : August 09, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, J​enista M​hagama
Responsive image

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, J​enista M​hagama,amewataka wadau wa kilimo kuwapatia ujuzi wa kutosha wakulima ili kukifanya kilimo kiweze kuwavutia vijana kuwekeza na kuongeza ajira pamoja na kasi yakuipeleka nchi katika viwanda.

Akizungumza jijini Arusha wakati akihitimisha maonesho ya 24 ya wakulima Nanenane kanda ya Kaskazini,Wazirii Jenista Mhagama,amesema kilimo kina uwezo wa kuajiri kundi kubwa ka vijana lakini maziingira yaliyopo yanawakatisha tamaa.

Baadhi ya washiriki wa maonesho ya wakulima Nanenane toka katika taasisi mbali mbali wamesema wametoa elimu kwa wakulima hasa wanaojishughulika na usindikaji mazao.

Kwa upande wa hifadhi za wanyama nchini,Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro,Rashid Taka,amesema kupitia maonesho hayo ya Nanene wananchi wanapaswa kutambua umuhimu wa hifadhi za wanyama nchini..

 Waliofanya vema katika maonesho hayo wamepata tuzo mbali mbali.

 

 

Sechelela Kongola             

 9/9/2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment