Responsive image
Responsive image
Posted : August 09, 2017 (6 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene
Responsive image

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene , amewaagiza wakuu wa mikoa kote Nchini, kuwafukuza kazi wakurugenzi na watendaji wengine wa Halmashauri wanaokaidi matakwa ya sheria kuondoa tozo kadhaa walizokuwa wakitozwa wakulima wanaposafirisha mazao kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Simbachawene ametoa agizo hilo wakati wa kilele cha Sikukuu ya wakulima, maarufu kama Nanenane, Kanda ya Nyanda za juu kusini, na kubaini kuwa kuna baadhi ya Halmashauri nchini, zimeendelea kuwatoza wakulima tozo ambazo zimeondolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

George Simbachawene amezikumbusha taasisi za serikali yakiwemo majeshi kuwa chachu ya mabadiliko kwa wananchi wanaoishi karibu na shughuli za uzalishaji wa mzao ya kilimo na mifugo, lakini akaipongeza pia mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini kuwa ghala la uhakika la Taifa.

Kutokana na kilimo, bado mkoa wa Mbeya umeendelea kushika nafasi ya tatu katika kuchangia pato la Taifa.

 

Hosea Cheyo          

 9/9/2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment