Responsive image
Responsive image
Posted : August 08, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina
Responsive image

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga  Mpina ameziagiza Halmashauri nchini kujenga mfumo wa kutibu maji taka katika machinjio ili kuondoa uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya machinjio pamoja na kuhifadhi ardhi oevu.

 

Mpina ametoa agizo hilo jijini Mwanza  wakati wa kukagua ujenzi wa mfumo wa kutibu maji taka katika machinjio ya Nyakato halmashauri ya jiji la Mwanza  unaotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi Milioni mia saba.

 

Mradi huo unatarajia kuondoa uchafuzi wa mazingira katika eneo la machinjio na pia katika ziwa Victoria kupitia mto nyashishi, ambao hupokea taka ngumu kutoka machinjioni baada ya kujengwa kwa mfumo wa kutibu maji taka.

 

Halmashauri nchini zimetakiwa kujenga mfumo wa kutibu maji taka ili kuhifadhi ardhi oevu.

 

 

REGINALD NDESIKA                   

AGOSTI 8, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment