Responsive image
Responsive image
Posted : February 12, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Rais wa zamani wa Liberia Ellen Sirleaf
Responsive image

Rais wa zamani wa Liberia Ellen Sirleaf ameshinda tuzo ya mwaka ya Mo Ibrahim Kwa Uongozi wa Afrika ambayo hupewa viongozi wa Afrika ambao wameonekana kuwa na utawala mzuri.

Sirleaf amekuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kushika nafasi ya Urais ambapo alianza mwaka 2006 na kumaliza muda wake mwezi uliopita baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.

Kamati ya Utendaji ya tuzo ya Mo Ibrahim imesema Sirleaf ameonesha uongozi wa kipekee katika kukabiliana na changamoto zisizowahi kutokea katika awamu zake mbili za uongozi alipokuwa Rais wa Liberia.

Wakati aliposhinda uchaguzi wa Rais nchini humo mwaka 2005, nchi hiyo ilikuwa imegawanyika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka kadhaa.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment