Responsive image
Responsive image
Posted : February 12, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Mkurugenzi wa Uchaguzi, NEC Ramadhani Kailima
Responsive image

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imesema maandalizi kwa ajili ya Uchaguzi mdogo katika majimbo ya Kinondoni jijini Dar es salaam, Siha mkoani Kilimanjaro na kata nane Tanzania bara yanaendelea vizuri

Akizungumza jijini Dar es salaam  mara baada ya mkutano wa Watendaji wa NEC na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni Aron Kagurumujuri, Mkurugenzi wa Uchaguzi,  Ramadhani Kailima amesema Tume inafuatilia kwa karibu maandalizi ya uchaguzi huo na tayari maafisa wa Tume wako maeneo yanayojiandaa kwa uchaguzi huo mdogo.

Kwa mujibu wa Kailima, Tume imejiridhisha kuwa maandalizi yanaendelea  vizuri na amepongeza jitihada zinazofanywa na Msimamizi wa Uchaguzi  jimbo la Kinondoni pamoja na Wasaidizi wake katika kuhakikisha changamoto zinazojitokeza zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Aidha amewashauri Wasimamizi wa Uchaguzi kuendelea kukutana na Wawakilishi wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya kutoa taarifa katika kila hatua ya kuelekea Uchaguzi huo kwa lengo la kuhakikisha kuwa vyama vinapata taarifa ya kila hatua ya maandalizi.

Katika hatua nyingine Kailima amesema NEC imejipanga kutoa vipindi vya Elimu ya Mpiga Kura mfululizo hadi siku ya Uchaguzi.

Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Majimbo ya Kinondoni jijini Dar es salaam  Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro na Udiwani katika Kata 8 za Tanzania Bara, unatarajiwa kufanyika  Jumamosi ijayo.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment