Responsive image
Responsive image
Posted : February 12, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Baadhi ya wachezaji wa Simba
Responsive image

Kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma amesema hawakutumia nguvu nyingi hapo jana kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gendarmerie ya Djibouti kwa sababu wanamichezo mingi mbele yao.

Djuma amesema kuwa ushindi walioupata unatosha na umewaweka kwenye nafasi nzuri huku kocha wa Gendarmerie, Mrundi  Issa Ivuyekure akisema timu yake ina wachezaji wengi chipukizi na kwamba alitaraja wangefungwa magoli mengi lakini ameona mabadiliko kwa soka la Djibouti.

Simba ambayo imerejea katika michuano ya kimataifa baada ya kukosekana kwa misimu zaidi ya mitano walionekana kuwa na kiu kubwa ya kupata ushindi kwenye mchezo huo na walianza kuandika bao la mapema kwenye dakika ya kwanza likifungwa na kiungo Said Ndemla kabla ya nahodha John Bocco kuifungia magoli mengine mawili katika dakika za 32 na 45 na kisha Emmanuel Okwi kukamilisha ushindi kwa bao la dakika ya 90.

Kwa matokeo hayo Simba wanahitaji sare pekee kwenye mchezo wa marudiano  ili kuweza kusonga mbele katika hatua ya kwanza na wakivuka basi watapambana na timu ya El Masry ya Misri  au Green Buffalos ya Zambia ambapo katika mchezo wa juzi baina ya timu hizo El Masry walishinda kwa bao nne kwa bila.

Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano hiyo ya kombe la shirikisho timu ya Zimamoto ya Zanzibar imeshindwa kutamba katika dimba la Amani kisiwani Unguja baada ya kulazimishwa sare ya bao moja kwa Moja na Wolaitta Dicha ya Ethiopia.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment