Responsive image
Responsive image
Posted : February 11, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini
Responsive image

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama cha Afican National Congress (ANC) cha Afrika Kusini leo Jumatatu kinatarajiwa kuketi na kufanya maamuzi kuhusiana na hatma ya Rais Jacob Zuma anayepambana na shinikizo kubwa ndani na nje ya chama chake, za kumtaka aachie madaraka ya Urais nchini humo.

Hilo linatokea wakati kukiwa na vikao kadhaa vya faragha vilivyofanyika kati ya Zuma na Makamu wa Rais Cyril Ramaphosa ambapo imeripotiwa kuwa Raamaphosa amefanya jitihada kubwa za kumshawishi Rais huyo aachie ngazi, lakini amekataa.

Vyama vya upinzani nchini humo vimeyakosoa mazungumzo ya faragha kati ya Ramaphosa na Zuma, vikisema kwamba bila shaka Zuma amekuwa akishinikiza kwamba angeweza tu kuachia madaraka kama atahakikishiwa kinga ya kutoshitakiwa, baada ya kufanya hivyo.

Upinzani nchini humo unataka Rais huyo aondolewe madarakani na kuwajibika kisheria moja kwa moja baada ya kufanya hivyo, kwa tuhuma za rushwa na ufisadi zinazomkabili.

Kwa upande wake, Ramaphosa amesema kuwa mazungumzo kati yake na Zuma yamekuwa yakifanyika kwa uangalifu mkubwa na kwa lengo moja kuu la kuwaunganisha Waafrika Kusini. 

Kuhusu kikao cha NEC kitachoketi leo, Ramaphosa amesema bila kufafanua zaidi, kwamba anaelewa waafrika kusini wanataka uongozi wa nchi hiyo kutatua mgogoro unaoukabiliana nao na kwamba kikao hicho cha NEC kitafanya hicho hicho kwa uhakika.  

ANC kilianzishwa mwaka 1912 kama chama cha wazawa wa Afrika Kusini kikiwa na lengo la kupigania haki za watu weusi na machotara hususan haki za kupiga kura lakini kuanzia mwaka 1940 kikajiwekea lengo thabiti la kuutokomeza mfumo mzima wa ubaguzi wa rangi (apartheid) uliosimikwa na walowezi wa kizungu nchini humo.

Chama hicho kimeendelea kutawala Afrika Kusini tangu kutokomezwa kwa ubaguzi wa rangi ambapo Rais wake wa kwanza Nelson Mandela alichaguliwa mwaka 1994.

Mnamo Desemba mwaka jana Rais na kiongozi mkuu wa ANC tangu mwaka 2007, Jacob Zuma, alipoteza nafasi yake kwenye chama ambapo sasa kinaongozwa na Makamu wa Rais, Ramaphosa.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment