Responsive image
Responsive image
Posted : February 10, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwajulia hali mabinti mapacha walioungana Consolata na Maria Mwakikuti katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Responsive image

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mwenyekiti wa Chama cha Walimu nchini (CWT) mkoa wa Singida Mwalimu Aron Jumbe aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), pamoja na kuwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa kwenye taasisi hiyo.

Waliojuliwa hali na Waziri Mkuu Majaliwa ni pamoja na mabinti mapacha walioungana Consolata na Maria Mwakikuti ambao nao wamelazwa katikaTaasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. 

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wagonjwa wengine na kuwaeleza kwamba Serikali ina dhamira ya dhati kuhakikisha inaboresha huduma za afya na kwamba madaktari wataendelea kuwahudumia vizuri ili kuhakikishia afya zao zinaimarika ili waweze kurejea katika shughuli zao za kila siku

Kwa upande wake Mwalimu Jumbe amemshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kwenda kumjulia hali. Pia amewashukuru madaktari na wauguzi wa (JKCI) kwa huduma nzuri wanazompatia tangu alipofika hospitalini hapo.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment