Responsive image
Responsive image
Posted : February 10, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
Responsive image

Wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam wameziomba mamlaka zinazohusika na utoaji haki kuharakisha utoaji wa haki hizo ili kusaidia wananchi wenye malalamiko ya muda mrefu kushughulikiwa.

Wakazi hao wametoa ombi hilo wakati wa kuhitimisha zoezi la kusikiliza malalamiko ya wananchi kwa ofisi ya mkoa wa Dar es salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amehitimisha zoezi hilo la kusikiliza malalamiko ya wananchi na maelezo ya  wanasheria 12 na kutaka kujua kwa kiasi gani viongozi wa ardhi katika manispaa mbalimbali za jiji la Dar es salaam wanawajibika ipasavyo.

Kwa upande wake Mwanasheria Mkoa wa Dar es salaam Fabiola Mwingira amepongeza zoezi hilo ambapo wananchi waliweza kutoa malalamiko yao na kuomba liwe endelevu.

Zaidi ya malalamiko 3000 ya wananchi 6052 yameshughulikiwa. 

LEVINA KATEULE

10 FEBRUARI 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment