Responsive image
Responsive image
Posted : February 10, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
Responsive image

Serikali imesema madai yote ya watumishi wa umma yaliyoonekana kuwa sahihi baada ya uhakiki  yatalipwa pamoja na mshahara wa mwezi huu. Madai hayo yanafikia Shilingi bilioni 43.39. 

Akizungungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philp Mpango amesema malipo hayo ambayo mengine yana zaidi ya miaka kumi yatahusisha mishahara isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu madaraka, nyongeza ya mishahara iliyotokana na kupandishwa vyeo na kuchelewa kurekebishiwa mishahara.

Amesema zoezi la  uhakiki wa madai hayo limeiwezesha serikali kuokoa Shilingi Bilioni 84.22 ambazo ni sawa na Asilimia 66 ya madai yote ya malimbikizo ya awali.

Waziri Mpango amesema serikali itaendelea kulipa madai ya watumishi kadri yanavyojitokeza ili kuondokana  na malimbikizo ambayo yanaweza kuisababishia serikali hasara kwa kulipa madai yasiyostahili.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment