Responsive image
Responsive image
Posted : February 10, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Mwenyekiti mpya wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Leodger Tenga
Responsive image

Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amemteua aliyewahi kuwa rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Leodger Chilla Tenga kuwa Mwenyekiti mpya  wa Baraza la Michezo la Taifa BMT, akichukua nafasi ya Dionis Malinzi ambaye muda wake umemalizika.

Tenga ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) ataongoza baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo akisaidiwa na wajumbe wapya sita wa Baraza hilo walioteuliwa na waziri huyo mwenye dhamana ya michezo.

Wajumbe hao ni Prof. Mkumbwa Mtambo, Bi. Beatrice Singano, Kanali Mstaafu Juma Ikangaa, John Ndumbaro, Rehema Madenge na Salmin Kaniki.

Aidha, Dkt. Mwakyembe amewateua wajumbe wengine watatu  wa Baraza hilo kutokana na nafasi za vyeo vyao ambao ni Yussuph Singo ambaye ni  Mkurungezi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt. Edicome Shirima ambaye ni Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia  na Mafunzo ya Ufundi na Mohammed Kiganja ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) .

Wakati huo huo Dkt. Mwakyembe  amemteua Timothy Mganga kuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo cha Malya kilichopo mkoani Mwanza, kwa kipindi cha miaka mitano.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment