Responsive image
Responsive image
Posted : February 09, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Yo-Jong
Responsive image

Dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Yo-Jong amewasili nchini Korea Kusini kwaajili ya kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa mashindano ya olimpiki ya majira ya baridi, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mwanafamilia wa Utawala wa Korea Kaskazini kutembelea nchi hiyo tangu mwaka 1950-1953 wakati wa vita vya Korea.

Katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo Korea Kaskazini na Korea Kusini watapeperusha bendera moja.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema hiyo ni ishara ya kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un  huenda yupo tayari kufanya mazungumzo ya amani na Korea Kusini.

Kim Yo Jong ana umri wa miaka 30 akizidiwa miaka minne na kaka yake.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment