Responsive image
Responsive image
Posted : February 09, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Mtendaji Mkuu wa AUB, Gregoire Ndjaka (aliyesimama) akizungumza na uongozi wa TBC Dar es Salaam Ijumaa, Februari 9, 2018
Responsive image

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) linatarajia kuhudhuria Mkutano wa  mwaka wa Umoja wa Mashirika  ya Utangazaji barani Afrika (AUB) ambapo pamoja na mambo mengine utajadili namna mashirika ya utangazaji yatakavyoweza kutangaza mashindano ya kombe la dunia  kwa gharama nafuu.

Mtendaji Mkuu wa AUB, Gregoire Ndjaka amesema mashirika mengi ya umma barani Africa ikiwemo TBC yanapata tabu kupata haki ya kurusha michuano hiyo kwasababu gharamu zake ni kubwa mno.

``Gharama za kutangaza kombe la dunia ni kubwa mno hivyo lazima tufanye kitu cha kuweza kuyasaidia mashirika ya utangazaji ya umma ili yaweza kutangaza michuano ya kombe la dunia ya mwaka huu`` alisema Ndjaka.

Naye Mkurugenzi  Mkuu wa TBC,  Dkt. Ayub Rioba amesema gharama ya sasa ya kurusha mpira huo ni kubwa hivyo mkutano huo utaleta unafuu kurusha matangazo hayo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa masoko wa TBC,  Daphrosa Kimbory amesema TBC inafanya kila jitihada kuhakikisha inatangaza mashindano ya Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika Julai Mwaka huu nchini Russia ambapo jumla ya timu 32 zitashiriki zikiwemo tano za Afrika ambazo ni Nigeria, Misri,Morocco,Tunisia na Senegal.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment