Responsive image
Responsive image
Posted : February 09, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Msemaji wa Simba, Haji Manara
Responsive image

Pendekezo lililotolewa na uongozi wa timu ya Simba likiwataka mashabiki wake kuwaunga mkono watani wao Yanga katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya St Louis United ya Shelisheli, limepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa timu hiyo.

Katika mitandao ya jamii, baadhi ya wachangajia mada waliodai kuwa ni mashabiki wa timu hiyo wamesema hawako tayari kuwashangilia Yanga katika mchezo wowote ule, ukiwemo huo dhidi ya St. Louis United utakaopigwa kesho kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam.

Wachangiaji mada wachache wameunga mkono pendekezo hilo ambapo katika majibizano ya hoja baadhi wamehoji kiwango cha 'Usimba' cha wale waliokubaliana na pendekezo hilo.

Akitoa pendekezo hilo, msemaji wa Simba, Haji Manara, amewataka mashabiki wa Simba na Yanga kubadilika ili waachane na mambo ya kizamani ya kuzomeana na sasa washirikiane katika michezo ya kimataifa ambapo timu zinapeperusha bendera ya Taifa.

Simba yenyewe itashuka dimbani Jumapili kucheza na timu ya Gendarmerie ya Djibouti katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika kwenye uwanja wa Taifa.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment